Saturday, April 30, 2016

Wavu wageukia ufukweni

Msdamsnasakl lkhlk hslahsajk hajk hsajk hk a jsjka
CHAMA cha Mpira wa Wavu Tanzania (TAVA) kimesema kuwa hivi sasa kipo katika mikakati ya kuhakikisha wanapata wachezaji wengi wa mchezo huo kwa upande wa ufukweni kutokana na idadi iliyopo kuwa ndogo nchini.

Mwenyekiti wa Tava, Agustino Agapa, ameliambia Dimba kuwa wameamua kufikia maamuzi hayo baada ya kuwepo kwa idadi kubwa ya wachezaji wa uwanjani tofauti na ilivyokuwa ufukweni.

Alisema ili mchezo huo ukuwe na kupendwa na watu hawana budi kuwa na idadi inayolingana kwa wachezaji wa ufukweni na wale wa uwanja wa kawaida.

“Ukiangalia idadi iliyopo sasa ya wachezaji wa wavu ufukweni ni ndogo na hii ni kutokana watu wengi kuona wanapoteza muda kwenda sehemu ambazo zinachezwa mchezo huo tofauti na ule mwingine ambao unaweza kucheza hata nyumbani kwako," alisema.

No comments:
Andika comments

Shukrani

Aina za Habari

Hifadhi