Saturday, April 30, 2016

RT waota medali Olimpiki Rio

kj dsakj dsakj hdsaj dhakskdsah dajkshdjhds a
SHIRIKISHO la Riadha Tanzania (RT) limesema vipaji na uwezo binafsi walionao wanariadha wao waliofuzu kushiriki michuano ya Olimpiki Rio 2016, vimewatia kiburi kuwa watarejea nchini na medali.

Kuelekea kwenye michuano hiyo itakayoanza Agosti mwaka huu, Tanzania itawakilishwa na wanariadha watatu waliofikia viwango vya kushiriki Olimpiki Rio.

Rais wa RT, Antony Mtaka, ameliambia Dimba kwamba Tanzania imechoka kuwa msindikizaji katika michuano hiyo hivyo ni wakati wa wanariadha hao kuwatoa kimasomaso kupitia vipaji na uwezo walionao.

Alisema licha ya ukata ambao ni tatizo kongwe katika vyama vya michezo, lakini maandalizi waliyofanya wanariadha hao yanatia moyo wa kwenda kupigania medali.

“Sasa Watanzania kuwa wasindikizaji imetosha, safari hii tunakwenda Brazil tukiwa na matumaini makubwa ya medali ni jambo linalowezekana iweje wenzetu waweze na sisi tushindwe?”alihoji bosi huyo wa RT.

Kwa takribani miaka 20 sasa Tanzania haijafanikiwa kurejea na medali katika michuano hiyo.

No comments:
Andika comments

Shukrani

Aina za Habari

Hifadhi