Showing posts with label Ufugaji wa Kuku. Show all posts
Showing posts with label Ufugaji wa Kuku. Show all posts

Monday, August 1, 2016

NaneNane Morogoro

Kuku wa Nyama wa Asili wenye Faida ni Kuchi.

    *Kuku hawa wanauwezo  wa           kuvumilia magonjwa.
    *Wanauzito mkubwa kulinganisha na aina yoyote ya kuku.

     *Nyama yake ni Tamu na Laini.

    *Ufugaji wa Kuku Huyu una Faida nyingi kwa mfugaji anayezalisha vifaranga kwa ajili ya uuzaji.

Kwa kujifunza zaidi tembelea Mabanda ya Halmashauri ya Handeni  na Halmashauri ya Ulanga ujifunze zaidi na kupata majogoo bora ya kuchi. #tusitawi Blog@NaneNane Morogoro 

Kuku aina ya Kuchi katika banda la Handeni. 
Kuku aina ya Kuchi mdomo kasuku katika banda la Ulanga. 

Sunday, May 22, 2016

Mgonjwa ya kuku

Kuku ni ndege rahisi kumfuga kwa ajili ya biashara. Kuku  akifugwa kitaalam anafaida kubwa.
Ufugaji bora wa kuku ni kukabiliana na magonjwa. Mfugaji anayeyajua magonjwa ya kuku mapema huokoa fedha ambazo angezipoteza iwapo kuku wake wangekufa.
Hatua  ya kwanza ni kuwachanja kuku wako. Chanjo muhimu ni hizi:
chanjo ya kuzuia kideli (newcastle). 

Vifaranga huchanjwa siku ya tatu mara tu baada ya kifaranga kutotolewa. Kisha hurudiwa siku ya 21 na baada ya hapo wachanje kuku wako kila baada ya miezi mitatu.

Kideli ni nini?
Kideli husababishwa na virusi.
Dalili za awali:
  • Kuku/Vifaranga hupata mafua makali hivyo kushindwa  kupumua  vizuri.
  • Kupata kikohozi
  • Kutokuwa na mate mdomoni ya utelezi na povu.
Dalili kwamba kuku wako ameshaelemewa na Kideli
  • Kuharisha choo cha kijani na njano
  • Kukohoa na kupumua kwa shida
  • Kuficha kichwa katikati ya miguu
  • Kukosa hamu ya kula na kunywa maji
  • Kutoa kamasi nyingi na  machozi wakati mwingine macho huziba kabisa
  •  Kuzungusha kichwa na kutembea kinyumenyume
  •  Vifo vya haraka
Kuwachanja kuku ndio kinga pekee
  • Watenge kuku wagonjwa kuzuia ugonjwa kuenenea Banda Zima.
    Epuka kuingiza kuku wageni
    Choma au fukie mizoga ya kuku waliokufa kwa ugonjwa
    Zingatia usafi wa mazingira

Wednesday, May 18, 2016

Ufugaji wa Kuku

Serikali ya George W. Bush ilifanya mpango ili watu wa ukoo wa Osama bin Laden waondolewe Marekani ili wasibughudhiwe. Machi 28, 2005, gazeti ‘Daily Time’s la Pakistan, likiripoti kutoka Washington DC., Marekani, lilidai kuwa FBI (Shirika la Upelelezi la Marekani) iliwasaidia Wasaudia kuondoka baada ya mashambulizi ya Septemba 11.”

Katika toleo lililopita tulilinukuu gazeti hilo lilisema hivi: “FBI walishiriki kikamilifu kuandaa ndege kwa ajili ya makumi ya raia wa Saudia—wakiwamo ndugu wa Osama bin Laden—baada ya mashambulizi ya kigaidi ya 9/11.”

Aina za Habari

Hifadhi