Sunday, May 22, 2016

Mgonjwa ya kuku

Kuku ni ndege rahisi kumfuga kwa ajili ya biashara. Kuku  akifugwa kitaalam anafaida kubwa.
Ufugaji bora wa kuku ni kukabiliana na magonjwa. Mfugaji anayeyajua magonjwa ya kuku mapema huokoa fedha ambazo angezipoteza iwapo kuku wake wangekufa.
Hatua  ya kwanza ni kuwachanja kuku wako. Chanjo muhimu ni hizi:
chanjo ya kuzuia kideli (newcastle)

Vifaranga huchanjwa siku ya tatu mara tu baada ya kifaranga kutotolewa. Kisha hurudiwa siku ya 21 na baada ya hapo wachanje kuku wako kila baada ya miezi mitatu.

Kideli ni nini?
Kideli husababishwa na virusi.
Dalili za awali:
  • Kuku/Vifaranga hupata mafua makali hivyo kushindwa  kupumua  vizuri.
  • Kupata kikohozi
  • Kutokuwa na mate mdomoni ya utelezi na povu.
Dalili kwamba kuku wako ameshaelemewa na Kideli
  • Kuharisha choo cha kijani na njano
  • Kukohoa na kupumua kwa shida
  • Kuficha kichwa katikati ya miguu
  • Kukosa hamu ya kula na kunywa maji
  • Kutoa kamasi nyingi na  machozi wakati mwingine macho huziba kabisa
  •  Kuzungusha kichwa na kutembea kinyumenyume
  •  Vifo vya haraka
Kuwachanja kuku ndio kinga pekee
  • Watenge kuku wagonjwa kuzuia ugonjwa kuenenea Banda Zima.
    Epuka kuingiza kuku wageni
    Choma au fukie mizoga ya kuku waliokufa kwa ugonjwa
    Zingatia usafi wa mazingira

1 comment:
Andika comments
  1. Nitalazimika kuanzisha ufugaji wa kuku maadamu darasa la ufugaji nitakuwa nalipata kupitia blogu hii.

    ReplyDelete

Shukrani

Aina za Habari

Hifadhi