Showing posts with label Utawala Bora. Show all posts
Showing posts with label Utawala Bora. Show all posts

Tuesday, June 28, 2016

DC Muhingo Atoa Darasa la Kustaafu

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Muhingo Rweyemamu ameeleza jinsi alivyofurahia kupumzika kazi hiyo ya Ukuu wa Wilaya.  Muhingo ameeleza hisia zake hizo katika ukurasa wake wa Face Book na hivi ndivyo alivyoandika:

"Mei 2012 niliteuliwa na mhe. JK kuwa DC Handeni. Nilipofika kule nikakuta watoto wanazuiwa kupata haki yao ya kuitwa watoto. Nilikuta watoto walio mashuleni wanapewa mimba hovyo na watoto wa miaka hata 12 wanaozwa. Niliandika hapa kwamba hata nikibaki peke yangu nitapambana. Niliwatoa watoto wengi kwenye ndoa na mmoja nilimfuata Bagamoyo. Mume wake alikuwa anapara samaki ferry.  Niliingia Handeni watoto wenye ujauzito wakiwa asilimia 11 kwa wanafunzi wa sekondari. Nimetoka 2015 mimba zikiwa asilimia. 0. 03.

Nilifika Handeni wananchi wakipelekewa chakula kila mwaka.  Nimetoka ikiwa ni ghala la taifa. Ghala ya NFRA iko pale Tengwe.

Niliingia Handeni misitu ikiwa ni shamba la bibi. Waulizeni TAFORI jina langu limeandikwa ofisini kwao kwa kurejesha miti ya asli. Nimeingia Handeni mauzo ghafi ya mifugo katika minada yakizalisha milioni 400 kwa mwezi. Nimetoka mauzo ghafi yamiwa bilioni 2 shilings. Ukweli ni kwamba hata nilipohamishwa kwenda Makete 2015 sikuondoka kinyonge. Nilisindikizwa na umati wa watu.

Makete nilikaa miezi mitano tu. Nilijipa kazi moja ya kuhakikisha madume bora ya ng'ombe wa Kitulo yanasambaa vijijini.  Tulifanikiwa.

Nimemalizia Morogoro napo kwa muda mfupi tu. Hata hivyo wananchi kote watanikumbuka kwa maamuzi ya haki.
Kwa uchache niyakumbuke hayo.

Namshukuru sana JK aliyeniteua na kunifanya niongeze ujuzi, busara na hekima katika maamuzi. Namshukuru sana JPM katika kpindi kifupi tukichokaa naye kama kamanda wetu.  Nafurahi kwamba alilipokea ombi langu la kustaafu. Naenda kujitegemea. Nimefurahi.

Mwisho niwapitishe katika darasa moja tunalopata toka Teabag yaani kile kifuko kibebacho majani ya chai. Kwanza hata mfuko wenyewe unajua kwamba what matters is what is inside the teabag. Utagundua kwamba teabags zinatengenezwa kwa marembo mengi. Kama zilivyo teabags ni sawa na sisi.

Vyeo vyetu, vyeti vyetu, magari tunayoendesha hakuna cha maana kama huduma kwa wananchi ni ya hovyo.

Ya pili the real flavour comes through only when the teabag gets into hot water. Na sisi bila kukumbana na misukosuko. Kama maji ya moto yanavyotumika kupima ubora wa majani, misukosuko inapima true character of a leader.

Tatu, teabag lazima iwe porous. Yaani iwe na matundu ya kuingiza maji ndani. Na sisi katika maisha huwezi kuishi in isolation. Kiongozi ni kazima awe mwangalifu asijenge kuta zinazowazuia wananchi kutufikia. Hakuna uongozi kama wananchi wanakuogopa.

Nne, mwisho wa yote kitu muhimu ni chai siyo teabag. Hakuna mtu anakunywa chai akasema wow hiyo ilikuwa teabag nzuri. Atasema that was a great cup of tea.  Na viongozi huwa tunajisahau na kudhani sifa tunapewa sisi kumbe ni huduma yako.

Mwisho kabisa na kwa mkazo:Eventually,  teabags need to make way and get out. Kwa bahati mbaya hapa huwa ni pagumu kwa viongozi. Wengi hujiiona kama wamekuwa katika utumishi uliotukuka na kwamba bila wao hakuna anayeweza kufanya kazi zao. Ukiangalia mfano wa teabag utagundua kwamba kuondoka ni muhimu na siyo muhimu tu bali pia ni lazima. Kama ni kiongozi au unatarajia kuwa,  unapoburudika na kikombe chako cha chai kumbuka darasa la teabag.
Tutaendelea kukutana hapa.

Nawashukuru kwa kupita hapa hata leo."

Tustawi Blog inamkaribisha Mhe. Muhingo Rweyemamu unaendelea kutoa Darasa hili la Kustaafu.

Wednesday, May 25, 2016

Waziri wa Elimu Avunja Bodi ya Vyuo Vikuu

http://www.jamiiforums.com/index.php?threads/1055316/
Breaking News : Serikali yavunja Bodi ya TCU,yawasimamisha kazi vigogo

Friday, May 20, 2016

Utawala Bora

Serikali ya George W. Bush ilifanya mpango ili watu wa ukoo wa Osama bin Laden waondolewe Marekani ili wasibughudhiwe. Machi 28, 2005, gazeti ‘Daily Time’s la Pakistan, likiripoti kutoka Washington DC., Marekani, lilidai kuwa FBI (Shirika la Upelelezi la Marekani) iliwasaidia Wasaudia kuondoka baada ya mashambulizi ya Septemba 11.”

Katika toleo lililopita tulilinukuu gazeti hilo lilisema hivi: “FBI walishiriki kikamilifu kuandaa ndege kwa ajili ya makumi ya raia wa Saudia—wakiwamo ndugu wa Osama bin Laden—baada ya mashambulizi ya kigaidi ya 9/11.”

Taarifa hiyo ilichapishwa pia katika gazeti ‘New York Times’ toleo la Jumapili iliyokuwa imepita, likitaja vyanzo vya serikali ya Marekani. ‘The Times’ lilisema nyaraka ilizozipata kutoka serikalini zinaonesha kuwa mawakala wa FBI walizilinda na kuzisindikiza familia mbili za Kisaudia kuondoka Marekani, na Wasaudia wengine waliruhusiwa kuondoka bila hata kupekuliwa au kuhojiwa.

Tulieleza pia kuwa ndege zilizowabeba raia hao wa Saudi Arabia ziliandaliwa baada ya tukio la Septemba 11 wakati kukiwa na madai kuwa kuna uhusiano na ushirika kati ya Rais George W. Bush na familia ya kifalme ya Saudi Arabia na ile ya bin Laden.

Aina za Habari

Hifadhi