
Monday, August 8, 2016

Tuesday, August 2, 2016

Wiki ya Unyonyeshaji Duniani
Nchi zaidi ya nchi 170 duniani zinasherehekea wiki ya unyonyeshaji kuanzia Agosti Mosi hadi Agost 7, ili kuchagiza jukumu la onyonyeshaji kwa lengo la kuboresha afya wa watoto kote duniani.
Kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO kunyonyesha ni njia bora ya kuwapatia watoto wachanga virutubisho muhimu na vya kipekee wanavyohitaji mwilini.
Shirika hilo linapendekeza watoto kupewa maziwa ya mama mara tu anapozaliwa kuanzia saa moja baada ya mtoto kuzaliwa hadi miezi sita.
Kunyonyesha sio tendo tu la kumpa mtoto chakula chake bali ni moja Wapo ya sehemu ya Malezi ya mwanzo.
Hata hivyo kwa Mujibu wa Utafiti uliofanywa na wizara ya afya nchini imebainika kuwa ni asilimia 51% tu ya watoto wenye umri wa Miezi 0 hadi sita wanaonyenyeshwa kikamilifu.
Tuesday, May 24, 2016

Hatua za Ukuaji wa Mimba
Kijusi (zygote)
Hatua ya kwanza huanza tangu yai la mama linapokutana na virutubisho toka kwa baba ambapo hutengenezwa kijusi (zygote).
Kuvunjwa vunjwa kwa seli hadi kukamilisha hatua ya kwanza, huchukua kipindi cha wiki kama mbili ndipo kijusi (zygote) hujikita vizuri katika mji wa mimba.
Kipindi hiki mwanamke anayetarajia mtoto akipima atagundulika kuwa ni mjamzito na hata yeye mwenyewe huweza kuhisi dalili za mabadiliko.
Kiini cha Mimba (embryo).
Tangu wiki ya nane (8) baada ya mimba kutungwa, kipindi hiki kiwango katika kugawanyika kwa seli kunaongezeka, mhimili wa kuzilinda hutengenezwa na viungo vinaanza kuonekana.
Wakati kijusi kikijishikishiza vizuri katika ukuta wa mji wa mimba, seli zake hutengeneza tabaka mbili. Kwa wakati huu kijusi hubadilika na kuwa kiini cha mimba (embryo).
Tabaka la ndani la kiini hiki hutengenezwa kuwa mfumo wa kumeng’enya chakula na mfumo wa hewa.
Tabaka la nje linatengenezwa kuwa mfumo wa fahamu, viungo vya hisia mbalimbali vya mwili huanza kuundwa.
Viungo vya hisia kama masikio, pua, macho na ngozi; nywele na kucha. Sehemu ya katikati hutengenezwa kuwa mifupa, misuli na mfumo wa uzazi. Kimsingi sehemu hii ya kiini cha mimba hutengezwa viungo vya
ndani ya mwili.
Yanayojiri katika Mji wa Mimba
Baada ya kutengenezwa kwa sehemu kuu tatu za kiini cha mimba, mfumo wa kusaidia ukuaji wa mtoto hutengenezwa sasa.
Mfumo huu ni pamoja na kondo la nyuma, kamba ya kitovu, ambayo huwa na mishipa miwili ya ateri na veini moja ambayo humuunganisha mtoto na kondo la nyuma na fuko la mimba ambalo ndilo hubeba yale maji ambayo ni maalumu kwa kumtunza mtoto hadi atakapozaliwa.
Kimsingi kabla hata mama mtarajiwa hajajua kama ni mjamzito, yote haya yanakuwa yemekuwa yamekwishafanyika katika tumbo lake. Katika wiki ya tatu uti wa mgongo wa mtoto huanza kutengenezwa.
Katika kipindi cha siku 21, macho huanza kutokeza na siku 24, seli za moyo huanza kujigawanya.
Katika wiki ya nne via vya uzazi huanza kujulikana kama ni Me au ni Ke na vifuko kwa ajili ya mikono na miguu kujitokeza.
Vyumba vinne vya moyo huanza kujitengeza na mishipa ya damu huanza kujitokeza.
Tangu wiki ya tano hadi ya nane mikono na miguu huanza kutofautiana na wakati huu pia uso unaaza kutokeza ingawa si rahisi kujulikana.
Itaendelea…..
Friday, May 20, 2016

Ujauzito
Ujauzito umekuwa ukichukuliwa kama jambo la kawaida.Kwa wanawake wengi ambao ni mara yao ya kwanza kuitwa mama na wanaume ambao pia ni mara yao ya kwanza kuitwa baba, jambo hili si la kawaida sana. Ni furaha isiyoelezeka.Hivyo basi Taarifa sahihi kwenu mnaopata mtoto kwa mara ya kwanza ni hatua ya kwanza ya malezi.
Malezi haya yanaanza na Wiki 36-40 za Ujauzito.Ndio Malezi ya Kibaolojia.
Fuatilia hapa kwa maelezo zaidi upate kujua zaidi

Malezi ya Kibaiolojia
Katika toleo lililopita tulilinukuu gazeti hilo lilisema hivi: “FBI walishiriki kikamilifu kuandaa ndege kwa ajili ya makumi ya raia wa Saudia—wakiwamo ndugu wa Osama bin Laden—baada ya mashambulizi ya kigaidi ya 9/11.”
Taarifa hiyo ilichapishwa pia katika gazeti ‘New York Times’ toleo la Jumapili iliyokuwa imepita, likitaja vyanzo vya serikali ya Marekani. ‘The Times’ lilisema nyaraka ilizozipata kutoka serikalini zinaonesha kuwa mawakala wa FBI walizilinda na kuzisindikiza familia mbili za Kisaudia kuondoka Marekani, na Wasaudia wengine waliruhusiwa kuondoka bila hata kupekuliwa au kuhojiwa.
Tulieleza pia kuwa ndege zilizowabeba raia hao wa Saudi Arabia ziliandaliwa baada ya tukio la Septemba 11 wakati kukiwa na madai kuwa kuna uhusiano na ushirika kati ya Rais George W. Bush na familia ya kifalme ya Saudi Arabia na ile ya bin Laden.