Tuesday, May 17, 2016

Simba na Yanga


“Ni kweli! Nisikilize mwanangu, wewe ni shujaa pekee kati yetu sisi wakimbizi, unaweza ukabadili taswira nzima ya maisha ya watu hapa Monja. Umesikia mwenyewe kuwa kabla ya sisi hatujaletwa hapa, maovu yaote yalikuwa yanatendeka bila kujali watu hawa ni binadamu na raia wa taifa hili.


Lakini tulipokuja sisi maisha yameanza kubadilika. Unakumbuka siku tatu zilizopita kamanda mkuu aliwasamehe wale watu waliotaka kutoloka hapa kambini wasiuawe?

Leo amewaadhibu wanajeshi wake hauoni hilo ni jambo zuri kwa upande wetu na hii yote kwa sababu anakupenda wewe. Sasa nachokuomba mwanangu jitahidi kuwa karibu naye ujifanye kama unamuelewa na akikutamkia anakupenda

usimkubalie ila onyesha kama utamkubalia kesho na kesho kutwa ili ajue kuwa anachokifanya kwa sasa wewe unakikubali. Hii itakuwa salama kwetu sisi na watoto wetu utakuwa umewaokoa watu wengi sana mwanangu, kamanda huyu roho yake imeshabadilika kwa kuwa amekuona wewe, na endapo hatakuona mbele yake moyo wake wa ukatili utamrudia tena. Hatuna njia nyingine y

a kujiokoa ila ni wewe mwanangu waokoe watu wa taifa lao ambao walishakosa matumaini na jeshi la serikali yao sawa mwanangu,” aliongea Isabella kwa msisitizo akimtazama mwanaye Leah ambaye alionyesha ujasiri na kuukubali ushauli wa mama yake.

No comments:
Andika comments

Shukrani

Aina za Habari

Hifadhi