Showing posts with label Ujauzito. Show all posts
Showing posts with label Ujauzito. Show all posts

Sunday, August 14, 2016

Vijimambo vya Ujauzito


Mambo Haya huwezi kuelezwa na daktari

Kipindi cha ujauzito kimejaa mambo mengi ya kustaajabisha. Lakini kwa akina mama watarajiwa kwa mara ya kwanza hujumuisha mambo ambayo hakuyatajaria kuwa ni ya kawaida katika kipindi hicho. Mambo haya pia si rahisi kuambiwa na daktari yeyote. Ila ni muhimu uyajue.

Kuwashwa tumboni
"Katika mwezi wa saba wa ujauzito wangu, nilipatwa na muwasho tumboni kiasi kwamba nilikuwa siwezi kuvumilia” anakumbuka Skola John

Wataalam wa afya ya uzazi na magonjwa ya akina mama wanasema kuwa hali hii inasababishwa na ukavu wa ngozi na kutanuka kwa ngozi kutokana na kukua kwa mtoto. Hivyo inashauriwa endapo utakutwa na hali hii usijikune sana kwani inaweza kusababisha upate alama za mikwaruzo  badala yake jitahidi kujipaka mafuta ya kuainisha ngozi mara kwa mara. Pendelea kupaka Mafuta ya nazi au olive oil.



Hata hivyo kipindi cha ujauzito akina mama wengi pia husumbuliwa na matatizo mbalimbali ya ngozi.Ni muhimu kuwa mwangalifu pindi uonapo dalili ambazo sio nzuri katika ngozi yako ukamuona daktari ambaye ni mtaalam wa mausala yanayohusu ngozi au uendepo kliniki muulize daktari wako akupe mwongozo mzuri wa uhakika.

Tuesday, May 24, 2016

Hatua za Ukuaji wa Mimba

Kijusi (zygote)

Hatua ya kwanza huanza tangu yai la mama linapokutana na virutubisho toka kwa baba ambapo hutengenezwa kijusi (zygote).

Kuvunjwa vunjwa kwa seli hadi kukamilisha hatua ya kwanza, huchukua kipindi cha wiki kama mbili ndipo kijusi  (zygote) hujikita vizuri  katika mji wa mimba.

Kipindi hiki mwanamke anayetarajia mtoto akipima atagundulika kuwa ni mjamzito na hata yeye mwenyewe huweza kuhisi dalili za mabadiliko.

Kiini cha Mimba (embryo).
Tangu wiki ya nane  (8) baada ya mimba kutungwa, kipindi hiki kiwango katika kugawanyika kwa seli kunaongezeka, mhimili wa kuzilinda hutengenezwa na viungo vinaanza kuonekana.
Wakati kijusi kikijishikishiza vizuri katika ukuta wa mji wa mimba, seli zake hutengeneza tabaka mbili. Kwa wakati huu kijusi hubadilika na kuwa kiini cha mimba (embryo).

Tabaka la ndani la kiini hiki  hutengenezwa kuwa mfumo wa kumeng’enya chakula  na mfumo wa hewa.

Tabaka la nje linatengenezwa kuwa mfumo wa fahamu, viungo vya hisia mbalimbali vya mwili huanza kuundwa.

Viungo vya hisia kama masikio, pua, macho na ngozi; nywele na kucha. Sehemu ya katikati hutengenezwa kuwa mifupa, misuli na mfumo wa uzazi. Kimsingi sehemu hii ya kiini cha mimba hutengezwa viungo vya
ndani ya mwili.

Yanayojiri katika Mji wa Mimba
Baada ya kutengenezwa kwa sehemu kuu tatu za kiini cha mimba, mfumo wa kusaidia ukuaji wa mtoto hutengenezwa sasa.

Mfumo huu ni pamoja na kondo la nyuma, kamba ya kitovu, ambayo huwa na mishipa miwili ya ateri na veini moja ambayo humuunganisha mtoto na kondo la nyuma na fuko la mimba ambalo ndilo hubeba yale maji ambayo ni maalumu kwa kumtunza mtoto hadi atakapozaliwa.

Kimsingi kabla hata mama mtarajiwa hajajua kama ni mjamzito, yote haya yanakuwa yemekuwa yamekwishafanyika katika tumbo lake. Katika wiki ya tatu uti wa mgongo wa mtoto  huanza kutengenezwa.

Katika kipindi cha siku 21, macho huanza kutokeza na siku 24, seli za moyo huanza kujigawanya.

Katika wiki ya nne via vya uzazi huanza kujulikana kama ni Me au ni Ke na vifuko kwa ajili ya mikono na miguu kujitokeza.

Vyumba vinne vya moyo huanza kujitengeza na mishipa ya damu huanza kujitokeza.

Tangu wiki ya tano hadi ya nane mikono na miguu huanza kutofautiana na wakati huu pia uso unaaza kutokeza ingawa si rahisi kujulikana.
Itaendelea…..

Aina za Habari

Hifadhi