“Ni kweli! Nisikilize mwanangu, wewe ni
shujaa pekee kati yetu sisi wakimbizi, unaweza ukabadili taswira nzima ya
maisha ya watu hapa Monja. Umesikia mwenyewe kuwa kabla ya sisi hatujaletwa
hapa, maovu yaote yalikuwa yanatendeka bila kujali watu hawa ni binadamu na
raia wa taifa hili.
Lakini tulipokuja
sisi maisha yameanza kubadilika. Unakumbuka siku tatu zilizopita kamanda mkuu
aliwasamehe wale watu waliotaka kutoloka hapa kambini wasiuawe?
Leo amewaadhibu
wanajeshi wake hauoni hilo ni jambo zuri kwa upande wetu na hii yote kwa sababu
anakupenda wewe. Sasa nachokuomba mwanangu jitahidi kuwa karibu naye ujifanye
kama unamuelewa na akikutamkia anakupenda
usimkubalie ila
onyesha kama utamkubalia kesho na kesho kutwa ili ajue kuwa anachokifanya kwa
sasa wewe unakikubali. Hii itakuwa salama kwetu sisi na watoto wetu utakuwa
umewaokoa watu wengi sana mwanangu, kamanda huyu roho yake imeshabadilika kwa
kuwa amekuona wewe, na endapo hatakuona mbele yake moyo wake wa ukatili
utamrudia tena. Hatuna njia nyingine y
a kujiokoa ila ni
wewe mwanangu waokoe watu wa taifa lao ambao walishakosa matumaini na jeshi la
serikali yao sawa mwanangu,” aliongea Isabella kwa msisitizo akimtazama mwanaye
Leah ambaye alionyesha ujasiri na kuukubali ushauli wa mama yake.
No comments:
Andika commentsShukrani