Katika toleo lililopita tulilinukuu gazeti hilo lilisema hivi: “FBI walishiriki kikamilifu kuandaa ndege kwa ajili ya makumi ya raia wa Saudia—wakiwamo ndugu wa Osama bin Laden—baada ya mashambulizi ya kigaidi ya 9/11.”
Taarifa hiyo ilichapishwa pia katika gazeti ‘New York Times’ toleo la Jumapili iliyokuwa imepita, likitaja vyanzo vya serikali ya Marekani. ‘The Times’ lilisema nyaraka ilizozipata kutoka serikalini zinaonesha kuwa mawakala wa FBI walizilinda na kuzisindikiza familia mbili za Kisaudia kuondoka Marekani, na Wasaudia wengine waliruhusiwa kuondoka bila hata kupekuliwa au kuhojiwa.
Tulieleza pia kuwa ndege zilizowabeba raia hao wa Saudi Arabia ziliandaliwa baada ya tukio la Septemba 11 wakati kukiwa na madai kuwa kuna uhusiano na ushirika kati ya Rais George W. Bush na familia ya kifalme ya Saudi Arabia na ile ya bin Laden.
Nyaraka hizo zilipatikana kupitia ‘Sheria ya Uhuru wa Habari’ nchini Marekani baada ya mashtaka kufunguliwa dhidi ya Wizara ya Sheria ya nchi hiyo. Mashtaka hayo yalifunguliwa na taasisi ya kisheria ya Marekani, ‘Judicial Watch’.
Wednesday, May 18, 2016
Zana za Kilimo
Habari inayofuata
Habari ya Awali
Habari ya Awali
Habari Iliyotangulia
Habari Inayofuata
Habari Inayofuata
Kuhusu Unknown
Kuhusu mhariri wa habari hii
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Andika commentsShukrani