Je, unatatizo la kukatika Nywele?
Je,umewahi kujiuliza kwa nini ukichana nywele zinabaki rundo kwenye kitana? kwa nini ukichana nywele zako zinapukutika na kudondondoka? Je wajua vile ulavyo ni muhimu zaidi?
Kukatika kwa nywele ni tatizo kwa watu wengi. Wengi wao pia huwa hawajui wafanye nini ili kurejesha uoto wa asili katika nywele zao. Sababu zipo nyingi na kubwa huwenda ikawa ni kukosekana kwa virutubisho muhimu mwilini au msongo wa mawazo.
Sitawi leo inakuletea namna bora kabisa ya kustawisha nywele zako kwa kutumia Beetroot. Beatroot ni maarufu kwa kuongeza damu mwilini kutokana na kuwa na uwingi wa madini chuma. Lakini leo Beatroot inakuongezea virutubisho ambavyo vitazuia nywele zako kukatika au kunyonyoka.
Beetroot ina vitamini C, madini ya Chuma, Vitamini B6, Magnesium na Potassium. Beetroot huondoa kabisa ukavu katika ngozi ya kichwa na hivyo kuzuia nywele kukatika. Kutokana na kuwa na virutubisho murua hivyo huifanya ngozi yako ya kichwa kuwa nyevu na yenye afya.
Sharubati (juice) ya beetroot pia ni nzuri kupunguza msongo wa mawazo. Kwa hiyo basi kama unakatika nywele kwa kuwa unamsongo wa mawazo basi Beetroot ni suluhisho lako.
Beetroot |
Zipo njia nyingi za kutumia beetroot kustawisha nywele.
Unaweza kula katika salad, au kunywa kama Sharubati. Sharubati ya Beetroot inawasidia watu wengi sana wenye tatizo la kukatika ama kunynonyoka nywele.
lakini pia unaweza kuchanganya Lettuce na Beetroot au ukachanganya Beetroot na karoti. Spinach na karoti pia ni nzuri sana katika kustawisha nywele.
Kula kama Salad, osha vizuri ondoa ganda la juu katakata vizuri vipande vidogo vidogo unaweza kuongeza veneger au unaweza kuongeza kajichumvi kidogo na pilipili manga au ladha yoyote uipendayo.
Salad ya Beetroot na Karoti |
Hivyo basi Beetroot ni kirutubisho asilia kabisa cha kuotesha nywele zinazokatika. Kukatika kwa nywele ni ishara kwamba unakosa virutubisho muhimu mwilini mwako. Vyakula asilia ni muhimu sana na vinasaidia kuzuia nywele kukatika hovyo.
Tukutane hapa wakati mwingine.
No comments:
Andika commentsShukrani