Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Muhingo Rweyemamu ameeleza jinsi alivyofurahia kupumzika kazi hiyo ya Ukuu wa Wilaya. Muhingo ameeleza hisia zake hizo katika ukurasa wake wa Face Book na hivi ndivyo alivyoandika:
"Mei 2012 niliteuliwa na mhe. JK kuwa DC Handeni. Nilipofika kule nikakuta watoto wanazuiwa kupata haki yao ya kuitwa watoto. Nilikuta watoto walio mashuleni wanapewa mimba hovyo na watoto wa miaka hata 12 wanaozwa. Niliandika hapa kwamba hata nikibaki peke yangu nitapambana. Niliwatoa watoto wengi kwenye ndoa na mmoja nilimfuata Bagamoyo. Mume wake alikuwa anapara samaki ferry. Niliingia Handeni watoto wenye ujauzito wakiwa asilimia 11 kwa wanafunzi wa sekondari. Nimetoka 2015 mimba zikiwa asilimia. 0. 03.
Nilifika Handeni wananchi wakipelekewa chakula kila mwaka. Nimetoka ikiwa ni ghala la taifa. Ghala ya NFRA iko pale Tengwe.
Niliingia Handeni misitu ikiwa ni shamba la bibi. Waulizeni TAFORI jina langu limeandikwa ofisini kwao kwa kurejesha miti ya asli. Nimeingia Handeni mauzo ghafi ya mifugo katika minada yakizalisha milioni 400 kwa mwezi. Nimetoka mauzo ghafi yamiwa bilioni 2 shilings. Ukweli ni kwamba hata nilipohamishwa kwenda Makete 2015 sikuondoka kinyonge. Nilisindikizwa na umati wa watu.
Makete nilikaa miezi mitano tu. Nilijipa kazi moja ya kuhakikisha madume bora ya ng'ombe wa Kitulo yanasambaa vijijini. Tulifanikiwa.
Nimemalizia Morogoro napo kwa muda mfupi tu. Hata hivyo wananchi kote watanikumbuka kwa maamuzi ya haki.
Kwa uchache niyakumbuke hayo.
Namshukuru sana JK aliyeniteua na kunifanya niongeze ujuzi, busara na hekima katika maamuzi. Namshukuru sana JPM katika kpindi kifupi tukichokaa naye kama kamanda wetu. Nafurahi kwamba alilipokea ombi langu la kustaafu. Naenda kujitegemea. Nimefurahi.
Mwisho niwapitishe katika darasa moja tunalopata toka Teabag yaani kile kifuko kibebacho majani ya chai. Kwanza hata mfuko wenyewe unajua kwamba what matters is what is inside the teabag. Utagundua kwamba teabags zinatengenezwa kwa marembo mengi. Kama zilivyo teabags ni sawa na sisi.
Vyeo vyetu, vyeti vyetu, magari tunayoendesha hakuna cha maana kama huduma kwa wananchi ni ya hovyo.
Ya pili the real flavour comes through only when the teabag gets into hot water. Na sisi bila kukumbana na misukosuko. Kama maji ya moto yanavyotumika kupima ubora wa majani, misukosuko inapima true character of a leader.
Tatu, teabag lazima iwe porous. Yaani iwe na matundu ya kuingiza maji ndani. Na sisi katika maisha huwezi kuishi in isolation. Kiongozi ni kazima awe mwangalifu asijenge kuta zinazowazuia wananchi kutufikia. Hakuna uongozi kama wananchi wanakuogopa.
Nne, mwisho wa yote kitu muhimu ni chai siyo teabag. Hakuna mtu anakunywa chai akasema wow hiyo ilikuwa teabag nzuri. Atasema that was a great cup of tea. Na viongozi huwa tunajisahau na kudhani sifa tunapewa sisi kumbe ni huduma yako.
Mwisho kabisa na kwa mkazo:Eventually, teabags need to make way and get out. Kwa bahati mbaya hapa huwa ni pagumu kwa viongozi. Wengi hujiiona kama wamekuwa katika utumishi uliotukuka na kwamba bila wao hakuna anayeweza kufanya kazi zao. Ukiangalia mfano wa teabag utagundua kwamba kuondoka ni muhimu na siyo muhimu tu bali pia ni lazima. Kama ni kiongozi au unatarajia kuwa, unapoburudika na kikombe chako cha chai kumbuka darasa la teabag.
Tutaendelea kukutana hapa.
Nawashukuru kwa kupita hapa hata leo."
Tustawi Blog inamkaribisha Mhe. Muhingo Rweyemamu unaendelea kutoa Darasa hili la Kustaafu.
No comments:
Andika commentsShukrani