Tulieleza pia kuwa ndege zilizowabeba raia hao wa Saudi Arabia ziliandaliwa baada ya tukio la Septemba 11 wakati kukiwa na madai kuwa kuna uhusiano na ushirika kati ya Rais George W. Bush na familia ya kifalme ya Saudi Arabia na ile ya bin Laden.
Nyaraka hizo zilipatikana kupitia ‘Sheria ya Uhuru wa Habari’ nchini Marekani baada ya mashtaka kufunguliwa dhidi ya Wizara ya Sheria ya nchi hiyo. Mashtaka hayo yalifunguliwa na taasisi ya kisheria ya Marekani, ‘Judicial Watch’.
Aliyekuwa mshauri wa Ikulu ya Marekani, Richard Clarke, alinukuliwa katika gazeti ‘The New York Times’ la Septemba 4, 2003 akisema alikubaliana na mpango huo kwa sababu FBI ilimfahamisha kwamba Wasaudia waliokuwa wakiondoka hawakuwa na uhusiano wowote na ugaidi; na kwamba Ikulu ilikuwa inahofia ulipizaji kisasi kwa magaidi ambao ungetokea ikiwa hawangeondoka Marekani.
Kitendo cha Clarke kukubali kuhusika kwa Ikulu ya Marekani katika kuwaruhusu Wasaudia kuondoka, ikiwa ni pamoja na wanafamilia ya Osama, kilimfanya Seneta Charles Ellis “Chuck” Schumer wa Jimbo la New York kuitaka Ikulu ya Marekani ifanye uchunguzi wa jambo hilo.
Wednesday, May 18, 2016
Maksai kwa ajili ya kilimo
Habari inayofuata
Habari ya Awali
Habari ya Awali
Habari Iliyotangulia
Habari Inayofuata
Habari Inayofuata
Kuhusu Unknown
Kuhusu mhariri wa habari hii
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Andika commentsShukrani