Ufugaji wa mbuzi wa kisasa |
Tulieleza pia kuwa ndege zilizowabeba
raia hao wa Saudi Arabia ziliandaliwa baada ya tukio la Septemba 11 wakati
kukiwa na madai kuwa kuna uhusiano na ushirika kati ya Rais George W. Bush na
familia ya kifalme ya Saudi Arabia na ile ya bin Laden.
Nyaraka hizo zilipatikana kupitia ‘Sheria
ya Uhuru wa Habari’ nchini Marekani baada ya mashtaka kufunguliwa dhidi ya
Wizara ya Sheria ya nchi hiyo. Mashtaka hayo yalifunguliwa na taasisi ya kisheria
ya Marekani, ‘Judicial Watch’.
Aliyekuwa mshauri wa Ikulu ya
Marekani, Richard Clarke, alinukuliwa katika gazeti ‘The New York Times’ la
Septemba 4, 2003 akisema alikubaliana na mpango huo kwa sababu FBI
ilimfahamisha kwamba Wasaudia waliokuwa wakiondoka hawakuwa na uhusiano wowote
na ugaidi; na kwamba Ikulu ilikuwa inahofia ulipizaji kisasi kwa magaidi ambao
ungetokea ikiwa hawangeondoka Marekani.
Kitendo cha Clarke kukubali kuhusika
kwa Ikulu ya Marekani katika kuwaruhusu Wasaudia kuondoka, ikiwa ni pamoja na
wanafamilia ya Osama, kilimfanya Seneta Charles Ellis “Chuck” Schumer wa Jimbo
la New York kuitaka Ikulu ya Marekani ifanye uchunguzi wa jambo hilo.
No comments:
Andika commentsShukrani