Wednesday, May 18, 2016

Ng'ombe wa maziwa

KATIKA matoleo mawili yaliyopita tulieleza kinaganaga kwamba Marekani haikuwahi hata siku moja kumtafuta Osama bin Laden, hususan kwa tukio la mashambulizi ya Septemba 11, 2001. Kama walikuwa wanamtafuta, kwanini waliiondoa familia yake nchini Marekani siku mbili tu baada ya kudai kuwa ndiye aliyeishambulia nchi hiyo?

Serikali ya George W. Bush ilifanya mpango ili watu wa ukoo wa Osama bin Laden waondolewe Marekani ili wasibughudhiwe. Machi 28, 2005, gazeti ‘Daily Time’s la Pakistan, likiripoti kutoka Washington DC., Marekani, lilidai kuwa FBI (Shirika la Upelelezi la Marekani) iliwasaidia Wasaudia kuondoka baada ya mashambulizi ya Septemba 11.”

Katika toleo lililopita tulilinukuu gazeti hilo lilisema hivi: “FBI walishiriki kikamilifu kuandaa ndege kwa ajili ya makumi ya raia wa Saudia—wakiwamo ndugu wa Osama bin Laden—baada ya mashambulizi ya kigaidi ya 9/11.”

Taarifa hiyo ilichapishwa pia katika gazeti ‘New York Times’ toleo la Jumapili iliyokuwa imepita, likitaja vyanzo vya serikali ya Marekani. ‘The Times’ lilisema nyaraka ilizozipata kutoka serikalini zinaonesha kuwa mawakala wa FBI walizilinda na kuzisindikiza familia mbili za Kisaudia kuondoka Marekani, na Wasaudia wengine waliruhusiwa kuondoka bila hata kupekuliwa au kuhojiwa.

No comments:
Andika comments

Shukrani

Aina za Habari

Hifadhi