Katika hali isiyo ya kawaida
Naibu Spika wa Bunge leo asubuhi aliliahirisha Bunge kabla ya muda wake baada ya wabunge kutaka kujadiliwa suala la wanafunzi wa UDOM kufukuzwa chuoni wakati hawana kosa.
Mwananchi imeandika,
Hatua hiyo imekuja baada ya Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari kuomba mwongozo na kutaka suala la wanafunzi hao lijadiliwe kama jambo la dharura linalopaswa kujadiliwa na Binge, badala yake Naibu Spika, Dr. Tulia Ackson alisema jambo hilo haliwezi kusitisha shughuli za Bunge hivyo haliwezi kujadiliwa kwa wakati huo.
Kauli hiyo iliwanyanyua wabunge wa upinzani na baadhi ya wa CCM wakipinga kauli hiyo huku wakiwa wamesimama jambo ambalo lilisababisha kuaihirishwa kwa Bunge hadi saa 10:00 jioni huku akiagiza kukutana kwa kamati ya uongozi ya Bunge.
Wanafunzi hao wapatao 7000 wameripotiwa na vyombo vya Habari hususan magazeti kuwa baada ya kufunuliwa chuoni hapo wameonekana wakingaika mjini Dodoma huku wengi wao wakiwa hawana nauli za kurejea makwao.
Vilevile vyombo hivyo vimewakariri baadhi ya wanafunzi wakisema wataishia kuwa machangudoa.
No comments:
Andika commentsShukrani