Serikali ya George W. Bush ilifanya
mpango ili watu wa ukoo wa Osama bin Laden waondolewe Marekani ili wasibughudhiwe.
Machi 28, 2005, gazeti ‘Daily Time’s la Pakistan, likiripoti kutoka
Washington DC., Marekani, lilidai kuwa FBI (Shirika la Upelelezi la Marekani) iliwasaidia
Wasaudia kuondoka baada ya mashambulizi ya Septemba 11.”
Katika toleo lililopita tulilinukuu gazeti
hilo lilisema hivi: “FBI walishiriki kikamilifu kuandaa ndege kwa ajili ya
makumi ya raia wa Saudia—wakiwamo ndugu wa Osama bin Laden—baada ya
mashambulizi ya kigaidi ya 9/11.”
Taarifa hiyo ilichapishwa pia katika
gazeti ‘New York Times’ toleo la Jumapili iliyokuwa imepita, likitaja
vyanzo vya serikali ya Marekani. ‘The Times’ lilisema nyaraka
ilizozipata kutoka serikalini zinaonesha kuwa mawakala wa FBI walizilinda na
kuzisindikiza familia mbili za Kisaudia kuondoka Marekani, na Wasaudia wengine
waliruhusiwa kuondoka bila hata kupekuliwa au kuhojiwa.
Tulieleza pia kuwa ndege zilizowabeba
raia hao wa Saudi Arabia ziliandaliwa baada ya tukio la Septemba 11 wakati
kukiwa na madai kuwa kuna uhusiano na ushirika kati ya Rais George W. Bush na
familia ya kifalme ya Saudi Arabia na ile ya bin Laden.
No comments:
Andika commentsShukrani